Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:06

Trump kutoa amri mpya ya uhamiaji


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump anategemewa kusaini amri mpya kuhusu wahamiaji Jumatatu baada ya mahakama ya rufaa kuzuia utekelezaji wa amri alioitoa mara ya kwanza.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinasema kuwa Iraq haitakuwa tena katika orodha ya nchi zilizokuwa zimeathiriwa na amri ya kwanza ya kuwazuia wahamiaji kutoka mataifa saba na mpango wa makazi ya wakimbizi.

Amri ya awali ya Trump iliosainiwa Januari 27 ilikuwa imezitaja nchi nyingine zaidi ya Iraq, zikiwemo Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen.

Katazo hilo lilisababisha mkang’anyiko mkubwa katika viwanja vya ndege ulimwenguni wakati maafisa wa uhamiaji walipokuwa wanawaza iwapo katazo hilo liliwahusisha watu wenye hati za kudumu- green cards na viza ambazo zilikuwa tayari zimeidhinisshwa.

Mahakama ya rufaa iliendeleza maamuzi ya mahakama ya serikali kuu ikitaka amri ya katazo la kusafiri la Trump lisimamishwe kwa muda, likihoji iwapo lilikuwa limetolewa kwa mujibu wa katiba.

Lakini uongozi ulisema kuwa rais anamamlaka ya kuilinda Marekani kutokana na uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi.

Japo kuwa rais ana mpango wa kurekebisha agizo la kiutendaji, White House inapingana na uamuzi wa mahakama ya rufaa, na wataalamu wa sheria wanasema mgogoro huu unaweza kuishia kupelekwa mbele ya Mahakama Kuu.

Aliyekuwa Waziri wa Usalama Michael Chertoff ameiambia VOA anamatumaini kwamba rais atakuja na amri ambayo “itakuwa na busara bila ya kuwaingiza watu wasiohusika katika katazo hilo la wahamiaji.”

XS
SM
MD
LG