Hatua hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa tarehe 19 mwezi Januari 2021.
Katika taarifa yake Jumapili, Pompeo amesema kuwaita magaidi waasi wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran pamoja na viongozi wa kundi hilo, ni kutaka wawajibishwe kwa vitendo walivyofanya, kama mashambulizi ya kuvuka mIpaka ambayo yalihatarisha usalama wa raia, miundombinu na usafirishaji wa kibiashara.
Pompeo amesema lengo pia ni kusaidia kufanikisha juhudi za kumaliza mzozo wa Yemen ulioanza mwaka 2014.
Mzozo huo ulianza pale waasi wa Kihouthi walipouteka mji mkuu wa Yemen, na kupambamoto mapema mwaka 2015 wakati kulipoanzishwa kampeni ya majeshi ya ushirika yalio ongozwa na Saudi Arabia ili kuwaondoa waasi hao na kurejesha serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa.