Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:10

Milipuko miwili yatokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden


Milipuko iliyotokea uwanja wa ndege wa Aden, Yemen, Disemba. 30, 2020.
Milipuko iliyotokea uwanja wa ndege wa Aden, Yemen, Disemba. 30, 2020.

Milipuko miwili imeripotiwa kuutuikisa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden, Yemen, Jumatano muda mfupi tu baada ya kuwasili ndege iliyokuwa inawasafirisha wajumbe wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa.

Afisa mmoja wa usalama ameliambia shirika la habari la Reuters kuna watu kadhaa waliojeruhiwa lakini hakuna afisa wa serikali miongoni mwao.

Serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa na wanaotaka kujitenga wa kusini wameunda serikali mpya ya kushirikiana madaraka hapo Disemba 18 na waliwasili katika mji huo wa kusini wa Aden Jumatano baada ya kuapishwa nchini Saudi Arabia.

Serikali hiyo yenye wajumbe 24 iliundwa chini ya usimamizi wa serikali ya Riyadh ambayo inaongoza muungano wa nchi za Kiarabu unaopambana na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran wanaoshikilia mji mkuu wa Sanaa tangu 2014.

Serikali hiyo mpya iliyoapishwa na Rais Abderabbo Mansour hadi siku ya Jumamosi imeundwa kupambana na uasi unaoendelea katika sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG