Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 12:24

Netanyahu aripotiwa kufanya ziara ya siri Saudi Arabia


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, kushoto, na mwana wa mfalme Mohammed bin Salman.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, kushoto, na mwana wa mfalme Mohammed bin Salman.

Vyombo vya Habari vya Israel vinaripoti kwamba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefanya ziara ya siri Jumapili kwenda Saudi Arabia kwa mazungumzo na mwana mfalme Mohammed bin Salman, pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo.

Ripoti zinasema ujumbe wa Israel pia ulimjumuisha Yossi Cohen, Mkuu wa Mossad, idara ya taifa ya upelelezi ya Israel na kuelezea data za ufuatiliaji wa safari ya ndege binafsi iliyokuwa ikisafiri kutoka Tel Aviv kwenda Neom, Saudi Arabia na kurudi saa kadhaa baadae.

Ofisi ya Netanyahu haikutoa maoni yeyote hadharani, juu ya safari ya aina hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje Marekani, haikujumuisha au kusema chochote kuhusu Netanyahu, katika taarifa yake ya Jumapili ya mkutano wa Pompeo na Mohammed bin Salman ambao ulifanyika huko Neom.

Walijadili juu ya haja ya umoja wa ghuba, kukabiliana na tabia ya kichokozi ya Iran katika eneo hilo, na umuhimu wa kufanikisha suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Yemen, Naibu msemaji wa wizara Cale Brown alisema.

XS
SM
MD
LG