Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:07

Watu 13 wauawa na wengine 50 kujeruhiwa katika milipuko miwili Aden


Milipuko iliyotokea uwanja wa ndege wa Aden, Yemen, Disemba. 30, 2020.
Milipuko iliyotokea uwanja wa ndege wa Aden, Yemen, Disemba. 30, 2020.

Karibu watu 13 wameuawa katika milipuko miwili inayo ripotiwa kuutikisa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden, kusini mwa Yemen, Jumatano muda mfupi tu baada ya kuwasili ndege iliyokuwa ina wasafirisha wajumbe wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa.

Ingawa hakuna kati ya maafisa hao wa serikali waliojeruhiwa lakini ina ripotiwa kuna zaidi ya watu 50 waliojeruhiwa na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Haijafahamika mara moja kilicho sababisha milipuko hiyo lakini milio ya bunduki ya hapa na pale ilisikika karibu na uwanja huo.

Serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa na wapiganaji wanaotaka kujitenga huko kusini wameunda serikali mpya ya pamoja kushirikiana madaraka hapo Disemba 18 na waliwasili katika mji huo wa kusini wa Aden Jumatano baada ya kuapishwa nchini Saudi Arabia.

Serikali hiyo ya wajumbe 24 iliundwa chini ya usimamizi wa serikali ya Riyadh ambayo inaongoza muungano wa nchi za Kiarabu unaopambana na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran wanaoshikilia mji mkuu wa Sanaa tangu 2014.

Serikali hiyo mpya iliyoapishwa na rais Abderabbo Mansour siku ya Jumamosi imeundwa kupambana na uasi unaoendelea katika sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi.

XS
SM
MD
LG