Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:15

Mapigano yanaendelea Yemen


Muungano wa wanajeshi unaoongozwa na Saudi Arabia na umoja wa falme za kiarabu, wanaopigana na waasi wa kihuthi wanaripotiwa kutekeleza shambulizi la angani dhidi ya sehemu za mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Shambulizi hilo limetokea saa chache baada ya kutokea milipuko kadhaa katika uwanja mkuu wa ndege katika mji wa Aden ulio kusini mwa Yemen, na kuua watu 26.

Muungano huo wa kijeshi ulianzisha mashambulizi usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sanaa, na katika sehemu mbili zikazoshikiliwa na wahouthi katika eneo la Rima Hamid, wilayani Sanhan, na Wadi Rjam katika wilaya ya Bani Hashish, kusini mwa Sanaa.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, amelaani shambulizi hilo baya dhidi ya uwanja wa ndege wa Aden, lililotokea mda mfupi baada ya ndege iliyokuwa imewabeba wajumbe wa baraza jipya la mawaziri linaloungwa mkono na Saudi Arabia, kutua.

Saa chache baada ya shambulizi hilo, mlipuko wa pili ulitokea karibu na makao ya rais katika eneo la Maasheq, karibu na mji wa Aden, ambapo mawaziri, waziri mkuu wa Yemen Maeen Abdulmalik, Pamoja na balozi wa Saudi Arabia nchini Yemen Mohammed Said al-Jaber, walikuwa wamepelekwa kwa ajili ya usalama wao.

Wafanyakazi wawili wa shirika la kutoa msaada la kimataifa la msalaba mwekundu wameuawa na mmoja hajulikani alipo.

Hakuna kundi la wapiganaji limedai kuhusika na shambulizi hilo hadi wakati tunaanda ripoti hii.

XS
SM
MD
LG