Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:10

Marekani na Iran zasema mazungumzo yao Vienna yanatija

Viongozi wa Mazungumzo ya Nyuklia, Naibu Katibu Mkuu Enrique Mora and Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje Abbas Araghchi wakisubiri kuanza mkutano wao Vienna, Apr. 6, 2021. (EU Delegation in Vienna/via Reuters)

Maafisa wa Marekani na Iran wanasema mazungumzo yao mjini Vienna, Austria, yanatija kufuatia mkutano wa pande hizo mbili Jumanne.  

Pande hizo mbili pamoja na watiaji saini wengine wa makubaliano ya mwaka 2015, juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, wanafanya kazi kufufua mpango huo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, Ned Price amesema hakuna matarajio ya mazungumzo ya moja kwa moja kwa wakati huu.

Lakini ameeleza kwamba Marekani ipo wazi kwa Iran kwa sababu "tupo wazi kwa diplomasia".

Anasema mkutano huko Vienna ni hatua inayoweza kuwa muhimu "tunapotaka kujua ni nini wa-Iran wapo tayari kufanya, ili kurudi kufuata makubaliano hayo ambayo yalipunguza mpango wa nyuklia wa Iran, baada ya kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo".

Marekani ilijitoa kwenye mkataba huo mwaka 2018 chini ya Rais wa wakati huo Donald Trump.

XS
SM
MD
LG