Mkurugenzi wa Kituo Maendeleo Endelevu ya Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Maryland, Nathan Hultman amesema mkutano wa viongozi kwa njia ya mtandao kuhusu mabadiliko ya hali ya Hewa utakua ni sherehe ya kurudi tena kwa Marekani kwenye jukwa la kimataifa.
Mkutano huo wa siku mbili umeitishwa na Rais Joe Biden na utahudhuriwa na darzeni ya viongozi wa dunia siku ya Alhamisi tarehe 22 April .
Baada ya miaka 4 ya suala hilo kupuuziwa na Marekani chini ya uwongozi wa rais wa zamani Donald Trump, mkutano huo wa kilele utakuwa “ni fursa kwa Marekani kurejea uwanjani kuonyesha inachukulia suala la mazingira kwa umakini mkubwa,” amesema David Waskow, mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha kupambana na mabadiliko ya hali ya Hewa, IKI.
Kituo hicho cha chja utetezi wa mazingira cha taasisi ya World Resources, hutoa msaada kwa mataifa yanayoendelea katika utafiti wa mazingira chenye makao yake Washington.
White House inasema itaangaza malengo makubwa kufikiwa 2030 kwa ajili ya kupunguza uchafuzi wa hewa kwa gesi za mkaa kabla ya mkutano huo wa kilele. Wanahaakti wanataka viwango vya uchafuzi huo vipunguzwe kwa asilimia 30 kutoka viwango vya 2005, “azma iliyo juu sana lakini bado” lengo “hilo linaweza kufikiwa,” Hultman amesema.
Na itaonyesha kwa wachafuzi wengine wakubwa kuwa mchangiaji mkubwa wa ongezeko la joto duniani yuko tayari kuchukua hatua.
“Bila shaka China inasubiri kuona nini Marekani itafanya,” Waskow amesema.
“Tunafahamu kuwa baadhi ya nchi nyingine --- Japan, Korea Kusini, Canada, India --- zinasubiri kuona ni hatua gani vipi Marekani itachukua.
Hatari zilizopo zinaongezeka na wataalam wengi wanasema miaka 2020 ni muongo unaotoa fursa ya ima kujenga au kubomoa.
.