Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:58

Volcano yalipuka Goma, wakazi wakimbilia Rwanda


Watu wakitathmini uharibifu uliosababishwa na mripuko wa volcano DRC
Watu wakitathmini uharibifu uliosababishwa na mripuko wa volcano DRC

Mlipuko wa Volcano kwenye mlima Nyiragongo mjini Goma umesababisha Maelfu ya watu kutoka Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kukimbilia Rwanda Jumamosi.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa takriban watu 3,000 kutoka DRC wamewasili Rwanda, vikinukuu mamlaka za uhamiaji nchini humo.

Taarifa zaidi zinaeleza waliowasili wamepewa hifadhi katika majengo ya shule na maeneo ya ibada ambayo yalianza kutayarishwa tangu taarifa za kutokea mlipuko wa Volcano.

Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Jenerali Constant Ndima amesema wakati hayo yakijiri mjini Goma, matope ya moto ambayo yamekuwa yakiteremka katika mlima Nyiragongo na kuishia nje kidogo ya mji wa Goma.

Kiongozi huyo amesema tathmini ya awali inaonyesha watu watano wamefariki hadi sasa.

Kulingana na Shirika la Habari la AFP watu wamerejea kwenye makazi yao mchana huu baada hatari hiyo ya matope ya moto kupungua kwa kiasi fulani.

Duru za habari zinaeleza kuwa walio wengi bado wana hofu ya kurejea na mamlaka za eneo hazijatoa taarifa yoyote rasmi tangu kulipopambazuka.

Mkazi mmoja anaeleza kuwa bado kuna harufu ya kemikali ya Sulphur ya tope la volcano na mlima Nyiragongo umesalia kuwa na rangi nyekundu inayoashiria Volcano bado inaripuka.

Vyanzo vya habari pia vimeeleza kuwa Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Congo(MONUSCO) imesema imefanya tathmini kwa njia ya anga katika mji wa Goma kujione hali ilivyo lakini hadi sasa. Matope ya Volcano hayajafika ndani ya mji huo lakini tahadhari kubwa inachukuliwa.

Taarifa pia zimeeleza kuwa Rais wa Congo Felix Tshisekedi amesema anakatisha ziara yake barani Ulaya na anarejea nyumbani kuratibu juhudi za misaada ya dharura.

XS
SM
MD
LG