Eneo la mauaji hayo kwa muda mrefu limeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama.
Hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa serikali katika eneo hilo.
Hilo ni tukio la pili la mauaji kama hayo mwezi huu.
Sheikh Moussa Djamali, alipigwa risasi alipokuwa akirejea jioni kutoka msikitini na mtu asiyejulikana, ambaye baadaye alitoweka, alisema Donat Kibuana, afisa wa utawala katika mji wa Beni alisema.
Mustapha Machongani, mwakilishi wa Beni wa Jumuiya ya Kiislamu ya Kongo, COMICO, alithibitisha mauaji hayo.
Tarehe mosi mwezi Mei, kiongozi mwingine wa Kiislam, imamu wa msikiti wa jiji, Sheikh Aliamini, aliuawa kwa njia hiyo hiyo, kwa mujibu wa Machongani.
Siku tano baadaye, utawala wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, uliweka Kivu Kaskazini, pamoja na jimbo jirani la Ituri, chini ya utawala wa kijeshi kwa siku 30, katika juhudi za kukabiliana na utovu wa usalama uliokithiri, katika eneo hilo.