Kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia imethibisha kutokea shambulizi hilo na kifo cha balozi.
Shambulizi limetokea karibu na mji wa Kanyamahoro mashariki mwa DRC, na inadaiwa kuwa washambuliaji walikuwa wakiuvizia msafara huo.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Gavana wa Jimbo la Kivu Kaskazini, Carly Nzanzu Kasivita, amesema kuwa balozi huyo alikuwa miongoni mwa msafara wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), wakiwa wanafanya ziara nje kidogo ya mji mkuu wa Goma, kutathimini hali ya usalama katika eneo hilo la mashariki mwa DRC.
Maafisa wa usalama wa mbuga ya wanyama ya Virunga, wamethibitisha kuwa balozi Luca Attanasio, ameuawa pamoja na mlinzi wake.
Makundi mengi ya waasi yamekuwa yakiendesha shughuli zao mashariki mwa DRC, hasa eneo ambalo lipo karibu na mpaka na mataifa ya Rwanda na Uganda.