Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:58

Wanamgambo washukiwa kuua raia 13 DRC


FILE - Wanamgambo, wakidaiwa kuwa na wapiganaji watoto, wenye silaha katika jamii ya Lendu wakilinda mkoa wa Ituri, DRC, Sept. 19, 2020.
FILE - Wanamgambo, wakidaiwa kuwa na wapiganaji watoto, wenye silaha katika jamii ya Lendu wakilinda mkoa wa Ituri, DRC, Sept. 19, 2020.

Wanamgambo wa Kiisilamu wanashukiwa waliwaua wanajeshi watatu na raia 13 na kuchoma moto kanisa walipovamia kijijini huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jimbo la Ituri kaskazini mashariki, jeshi na kikundi cha haki za binadamu wameeleza Jumatatu.

Washambuliaji hao walifyatua risasi walipoingia katika kijiji cha Ndalya Jumapili asubuhi, kusini mwa mji wa Bunia, alisema Christophe Munyanderu, mratibu wa kundi la Convention for the Respect of Human Rights.

Tathmini ya awali ilionyesha kuwa raia 13 waliuawa na washambuliaji hao na pia waliteketeza kanisa Katoliki, alisema.

Kwa sasa wanajeshi wetu wamekamata kijiji hicho baada ya shambulio hili ambalo liligharimu maisha ya raia, alisema msemaji wa jeshi Jules Ngongo Tshikudi, na kuongeza kuwa wanajeshi watatu na washambuliaji wanne waliuawa wakati jeshi lilipowarudisha nyuma.

Haikufahamika ni nani aliyefanya shambulio hilo, ingawa Tshikudi alilaumu wapiganaji wa Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye silaha la Uganda lililokuwa likifanya harakati zake mashariki mwa Congo tangu miaka ya 1990.

XS
SM
MD
LG