Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:58

Waasi wa ADF wameua watu 25 DRC


Wanajeshi wa DRC
Wanajeshi wa DRC

Raia 25 wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na mashambulizi ya waasi wanaoripotiwa kuwa wa kundi la Allied democratic forces, ADF.

Mkuu wa utawala katika mji wa Beni Donat Kibuana, amesema kwamba wanajeshi wamepata miili ya watu 25 wakati walipokuwa wanawasaka waasi wa ADF, jana alhamisi.

Waasi wa ADF, kutoka Uganda, ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi mashariki wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo tangu maiaka ya 1990, ni miongoni mwa makundi ya waasi 100 yanayopatikana mashariki mwa DRC.

Mashambulizi ya makundi ya wapiganaji yamekuwa yakiendelea mashariki mwa DRC kwa mda mrefu.

Sehemu hiyo imetengwa na serikali kuu ya Kinshasa kwa mda mrefu.

Mwezi July mwaka uliopita, maafisa wa Umoja wa mataifa walisema kwamba mashambulizi hayo huenda yanafikia uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kulingana na umoja wa mataifa, zaidi ya raia 1,000 wameuawa na kundi la ADF kati ya mwaka 2019 na 2020.

XS
SM
MD
LG