Gavana wa Kivu kaskazini huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC anawaomba wananchi wote pamoja na vijana kuunga mkono juhudi za wanajeshi wanao pambana na waasi wanaoshukiwa kuwa ni ADF huko eneo la Beni kwa kuwa jeshi pekee haliwezi kumaliza vitendo vya uasi bila kupata mchango kamili wa wananchi waliopo katika eneo.
Mwandishi wa VOA, Austere Malivika anaripoti zaidi kutoka Goma.