Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:13

Mgogoro wa kisiasa waendelea DRC, Tshisekedi ahutubia bunge


Rais wa DRC Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi

Baadhi ya wanasiasa waliokuwa wanamuunga mkono rais Mstaafu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wameeleza kumuunga mkono rais wa sasa Felix Tshisekedi.

Wanasiasa hao wameanza kujiondoa kutoka vyama vyao vya kisiasa na kujiunga na chama kipya cha rais Tshisekedi cha muungano wa taifa.

Chama hicho kiliundwa masaa machache baada ya Tshisehedi kutangaza kuvunja makubaliano kati yake na Kabila wiki iliyopita, akitaja tofauti ya kimaono namna ya kuendesha serikali.

Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali ya DRC kuunga mkono rais Tshisekedi huku jumuiya ya kimataifa ikitaka pande husika katika mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo kujadiliana na kuhakikisha kuna utulivu.

Viongozi wa chama cha kabila cha PPRD kama Kambere Kalumbi anamtaja rais Tshisekedi kama dikteta na kwamba hawatakubali.

Akihutubia Bunge hii leo, rais Tshisekedi amesema kwamba lengo kubwa la kuunda muungano kati yake na Kabila lilikuwa kuleta maendeleo lakini baadhi ya watu wameuvuruga muungano huo na kukosa kutimiza malengo yake ndio maana ameuvunja na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Tshisekedi ana matumaini kwamba serikali atakayounda itatimiza maslahi ya taifa akisitiza kwamba atafanya kazi na wale ambao wapo tayari kushirikiana naye.

Imetayarishwa na Austere Malivika, VOA, Goma

XS
SM
MD
LG