Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:09

Mshindi wa tuzo ya Nobel asisitiza uangalifu zaidi wa maambukizi ya Ebola


Dkt. Denis Mukwege
Dkt. Denis Mukwege

Kuibuka tena kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kumepokelewa kwa masikitiko makubwa na Dkt. Denis Mukwege mshindi wa tuzo ya Nobel ya mwaka 2018.  

Kuhusiana na Ebola, nina amini lazima tuongeze uangalifu wetu kuhusu virusi hivi. Tayari tumezidiwa na maambukizi ya virusi vya corona, na ikiwa Ebola inaongezeka tena wakati tayari tunateseka, hali inaweza kuwa ngumu sana kwa watu wa mashariki mwa nchi. Pendekezo pekee ambalo ninaweza kutoa kwa wakazi ni kwamba tuwe waangalifu zaidi juu ya ishara za Ebola na Corona, na iwapo tukishuku mtu yoyote ambaye mwili wake utaoneysha ishara za magonjwa hayo tuzigeukie taasisi za afya na kuzitaarifu mapema ili zijaribu kuleta suluhisho kwa tatizo hilo. Hii ndiyo njia pekee ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu,” alisema Dkt. Mukwege.

Ugonjwa huo umeripotiwa katika mji wa Butembo mashariki mwa DRC tangu mwanzoni mwa Februari.

FILE - Picha ya kijana akipatiwa chanjo ya Ebola Nov. 14, 2019, huko North Kivu, Goma, DRC.Picha kwa hisani ya Madaktari Bila Mipaka (MSF)
FILE - Picha ya kijana akipatiwa chanjo ya Ebola Nov. 14, 2019, huko North Kivu, Goma, DRC.Picha kwa hisani ya Madaktari Bila Mipaka (MSF)

Dkt Mukwege amesema hayo mjini Bukavu katika jimbo la Kivu Kusini wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hospitali yake ya Panzi, ndani ya mtaa wa Ibanda.

Ugonjwa wa Ebola umeripotiwa tena huko Butembo ikiwa imepita miezi takriban minane baada ya kutangazwa kumalizika kwa ugonjwa huo nchini Congo.

Hivi sasa visa vinne vimethibitishwa na maafisa wa afya katika eneo hilo. Licha yakuwa ugonjwa huo hivi sasa uko katika mji wa Butembo, viongozi wa Kivu Kusini wamechukua hatua muhimu kuhamasisha wakazi wa jimbo hilo kujikinga na maambukizi.

Pia alielezea kuwa hospitali ya Panzi imesaini mkataba na Japani ili kusaidia kutibu wagonjwa hususan waathirika wa dhuluma za ngono na ubakaji.

Kampeni ya chanjo imezinduliwa huko Butembo tangu Februari 15, hasa kwa madaktari wa hospitali ya Matanda ambako kuliripotiwa kisa cha kwanza cha Ebola mwezi Februari.

Tangu mwanzo wa wiki hii, dawa inayoitwa Ebanga imekubaliwa na viongozi wa Congo na imefikishwa Butemboili kusaidia katika matibuba. Hii ikiwa ni tiba moja ya sindano iliyoidhinishwa na shirika la Marekani linalosimamia ubora wa huduma ya Chakula na Dawa (FDA). Tiba ya Ebanga ni kwa ajili ya wote watu wazima na watoto. Ilianzishwa na daktari wa virusi Jean-Jacques Muyembe. Na ilikuwa katika majaribio tangu mwaka 2018.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Mitima Delachance, Bukavu, DRC.

XS
SM
MD
LG