Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:56

Mlipuko mpya wa Ebola umetangazwa nchini Guinea


Mfano wa kirusi cha Ebola
Mfano wa kirusi cha Ebola

Wizara ya Afya Guinea inasema wagonjwa waliumwa huku wakiharisha, kutapika na kutokwa na damu baada ya kuhudhuria mazishi katika wilaya ndogo ya Goueke. Watu walionusurika wametengwa katika vituo vya matibabu

Guinea imetangaza Jumapili mlipuko mpya wa Ebola baada ya vipimo vya watu watatu waliofariki na wanne walioumwa kusini mashariki mwa nchi hiyo, kuthibitisha kwamba watu hao walikua na virusi vya Ebola. Mlipuko wa kwanza wa Ebola ambao ulikua mlipuko mbaya zaidi duniani ulitokea nchini Guinea kati ya mwaka wa 2013 na 2016.

Wagonjwa waliumwa huku wakiharisha, kutapika na kutokwa na damu baada ya kuhudhuria mazishi katika wilaya ndogo ya Goueke. Wale walionusurika wametengwa katika vituo vya matibabu, wizara ya afya imesema.

Ikikabiliwa na hali hii na kwa mujibu wa kanuni za kimataifa za afya, serikali ya Guinea imetangaza janga la Ebola, wizara ya afya imesema katika taarifa.

Mtu aliyezikwa tarehe 1 Februari, alikua muuguzi katika kituo cha afya cha kieneo na alifariki baada ya kuhamishwa kwa ajili ya matibabu huko Nzerekore, mji ulio karibu na mpaka wa Liberia na Ivory Coast.

Mlipuko wa kwanza wa Ebola huko Afrika magharibi wa mwaka 2013 na 2016 ulianzia Nzerekore, shughuli nyingi za biashara kwenye mipaka ilio karibu zilikwamisha juhudi za kudhibiti virusi hivyo.

Wakati huo, virusi hivyo vya Ebola viliuwa takriban watu 11,300 kesi nyingi ziliripotiwa nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone.

XS
SM
MD
LG