Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:56

Mlipuko Mpya DRC : Wagonjwa 9 wa Ebola waripotiwa Ituri


A health worker wearing a protective suit enters an isolation pod to treat an Ebola patient at a treatment center in Beni, Democratic Republic of the Congo, July 13, 2019.
A health worker wearing a protective suit enters an isolation pod to treat an Ebola patient at a treatment center in Beni, Democratic Republic of the Congo, July 13, 2019.

Kitengo kinachopambana na ugonjwa wa Ebola katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa DRC kinasema visa vingine 9 vya ugonjwa huo vimepatikana katika kijiji cha Butama.

Daktari Jean Christophe Shako ambaye anaongoza juhudi za kupambana na Ebola Ituri, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba wagonjwa hao ni wale waliopinga kupewa chanjo dhidi ya Ebola, baada ya kushika kwa mkono maiti za ndugu zao waliofariki kutokana na Ebola. Anakiri kuwa wamekuwa na changamoto kubwa kutokomeza Ebola katika kijiji hicho cha Butama.

“Wakazi wa Butama hawaamini kabisa kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola, na hii ni kwa sababu ya kupotoshwa na watu waliotokea katika mji wa Butembo, ulioathiriwa zaidi na Ebola.”

Daktari Shako anasema wanajifunza mikakati mipya ya kupambana na Ebola katika kijiji cha Butama na vitongoji vingine vya mkoa wa Ituri.

“Inabidi tushirikiane na vijana na viongozi wa mitaa kwa kuwapa mafunzo kuhusu dalili za Ebola na mavazi maalum wanaopaswa kuvaa wakati wakuzika watu waliofariki kutokana na Ebola.”

Tangu Ebola kulipuka DRC mwezi Agosti mwaka jana, Zaidi ya visa elfu 3 vya Ebola vimethibishwa, na vifo Zaidi ya elfu 2 vimeripotiwa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Patrick Nduwimana, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG