Kwa mujib wa shirika la habari la AFP, linaripoti kuwa kamati ya kupambana na Ebola – Multisectoral Committee for Epidemic Response (CMRE) inasema visa 10 vimeripotiwa Jumatano katika kijiji cha Mabalako katika jimbo la Kivu Kaskazini, baada ya visa vingine 6 vimeripotiwa Jumanne.
Taarifa zimeongeza kuwa wa tatu miongoni mwa wagonjwa 6 ni waganga wa kienyeji.
Zaidi ya watu 2,200 wamefariki tangu Ebola ilipozuka nchini DRC mwezi Agosti mwaka wa 2018.
Kamati ya CMRE inasema, mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa afya yanayoendeshwa na makundi yenye silaha na vijana wenye hasira yamekwamisha juhudi za kupambana na Ebola, katika miji ya Beni, Biakato na Mangina.