Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:59

Pyongyang yapuuzia muelekeo wa Biden mpya wa diplomasia


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong

Korea Kaskazini imemkosoa Rais Joe Biden wa Marekani kuwa nchi yake itakabiliwa na “hali mbaya zaidi,” baada ya White House kutangaza muongozo mpana wa mpango wake wa kidiplomasia pamoja na Pyongyang.

Taarifa iliyotolewa Jumapili na mwanadiplomasia mwandamizi wa Korea Kaskazini, ilikuwa ni jibu la kwanza rasmi la nchi hiyo baada ya kuijadili sera ya uongozi wa Biden iliyokamilishwa hivi karibuni, inayoeleza uwazi wa kufanya mazungumzo na nchi hiyo yenye kujihami kwa silaha za nyuklia.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Kwon Jong Gun, mkurugenzi mkuu wa Idara ya masuala ya Marekani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Kaskazini, alitupilia mbali muelekeo uliotangazwa na Marekani kama “ni kificho cha kuendelea kuficha vitendo vyake vya uchokozi” dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea.”

“Ilivyokuwa hivi sasa… muhtasari wa sera mpya ya Marekani kwa DPRK imewekwa wazi, tutalazimika kushinikiza hatua zinazo lingana na hizo, na baada ya muda Marekani itajikuta katika hali ya mbaya zaidi,” Kwon amesema, kwa mujibu wa Shirika la Habari la serikali ya Korea.

“Marekani itakabiliwa na mgogoro utakaoendelea kuwa mbaya zaidi endapo hawataweza kuudhibiti katika siku za usoni iwapo imejiandaa kuendeleza mahusiano na DPRK-US, ikiendelea kujikita katika maoni na mtizamo wa sera zilizopitwa na wakati za zama za Fikra za Vita Baridi,” ameongeza.

Kufuatia mwezi mzima wa kupitia mpango huo, White House Ijumaa imetangaza mpango wa jumla kuhusu Korea Kaskazini. Ni sera ya kujaribu kuchukua mwelekeo wa kati na kati ukilinganisha na wale watangulizi wa karibuni wa Biden.

“Sera yetu haitajikita katika kufikia makubaliano makubwa, na wala hautategemea mkakati wa kusubiri,” amesema msemaji wa White House Jen Psaki. “Sera zetu zinataka urekebishaji, mwelekeo unaotekelezeka ambao uko wazi na utakao tafuta njia ya kuwepo diplomasia na DPRK na kuweza kupiga hatua zitakazo ongeza usalama wa Marekani, washirika wetu na majeshi yetu yaliyoko katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG