Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:09

Marekani, Korea Kusini yachelewesha mazoezi ya kijeshi yanayokosolewa na Korea Kaskazini


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper, kulia, na Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini Jeong Kyeong-doo, wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari Bangkok, Thailand Jumapili Nov. 17, 2019.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper, kulia, na Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini Jeong Kyeong-doo, wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari Bangkok, Thailand Jumapili Nov. 17, 2019.

Marekani na Korea Kusini wametangaza Jumapili wataahirisha mazoezi ya kijeshi yalioandaliwa kufanyika siku zijazo katika juhudi za kuimarisha kufanyika kwa mazungumzo ya amani na Korea Kaskazini yaliositishwa.

Hata hivyo Washington imekanusha kuwa hatua hiyo inapelekea kuiridhisha Pyongyang kukubali kurejea katika mazungumzo.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper amesema majeshi ya Marekani na Korea Kusini yatakuwa katika hali ya utayari wa hali ya juu pamoja na kuwepo kuahirishwa huko kwa mazoezi hayo, na amekanusha kuwa hatua ya kuahirisha mazoezi hayo ni kuiridhisha Korea Kaskazini.

Mazoezi hayo, yanayo julikana kama tukio la mafunzo ya mapambano ya angani, yangehusisha mfano wa mashambulizi ya angani na kuhusisha idadi isiyojulikana ya ndege za kivita kutoka Marekani na Korea Kusini.

Kwa kuzingatia wasiwasi wa Pyongyang, idadi ya mazoezi hayo yalikuwa yamepunguzwa kwa ukubwa na upeo wake tangu miaka iliyopita, lakini bado Korea Kaskazini ilikuwa inayapinga pamoja na yote hayo kufanyika.

Mapema mwezi huu, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini alilaumu mazoezi ya kijeshi ya angani yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini “kuzima” mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea na Washington.

Pyongyang imekuwa mara zote ikipinga mazoezi haya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini, wakiyatizama kama ni matayarisho ya uvamizi wa kijeshi katika nchi yao.

XS
SM
MD
LG