Trump alitoa maoni hayo mjini Tokyo akiwa na Waziri Mkuu wa Japan, ambaye anamtizamo tofauti juu ya kurushwa makombora hayo, kama alivyoripoti mwandishi wa VOA.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa hakuna shaka kwamba Korea Kaskazini imejaribu makombora matatu ya balistika ya masafa mafupi mapema mwezi huu.
Satellite ya kibiashara imeonyesha picha ya alama ilioachwa na moshi angani uliotokana na makombora hayo.
Lakini hata hivyo ukisikiliza maoni ya Rais Donald Trump wakati wa ziara yake ya kiserikali Japan, hutotambua kabisa kwamba makombora hayo yalirushwa.
Donald Trump alisema kuwa : Ni siku nyingi sasa. Hapakuwa na jaribio la roketi. Hapakuwa na jaribio la silaha ya nyuklia. Kumekuwa na harakati chache kutoka katika eneo hilo.”
Trump aliendelea kupinga wafanyakazi wake, ambao wanasisitiza kuwa jaribio la makombora linakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.