Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:13

Trump aanza ziara ya kiserikali Japan


Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Taro Kono (kushoto) na mkewe Kaori Kono wakimpokea Rais Donald Trump (kulia) na mkewe Melania Trump walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haneda Mei 25, 2019, in Tokyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Taro Kono (kushoto) na mkewe Kaori Kono wakimpokea Rais Donald Trump (kulia) na mkewe Melania Trump walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haneda Mei 25, 2019, in Tokyo.

Rais wa Marekani Donald Trump amewasili Japan, Jumamosi, kwa ziara ya kiserikali ya siku nne itakazipa uzito sherehe na michezo, japokuwa afisa wa ngazi ya juu wa White House ameahidi “ kutakuwa na mambo muhimu ya kutangaza.”

Ziara itaangaza fursa za kupiga picha kuliko kufanya makubaliano inaweza kuwa ni jambo la kusudi lililoandaliwa na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, ambaye amejenga uhusiano wa karibu na Trump. Wawili hao wamekutana au kuzungumza zaidi ya mara 40, kitu ambacho hakijawahi kutokea kabisa na viongozi wengine,” kwa mujibu wa White House.

Profesa katika Chuo Kikuu cha Keio Tomohiko Taniguchi, mwandishi mkuu wa hotuba za waziri mkuu zinazohusu sera za kigeni, anafikiria kuwa mbali na upande wa tafrija wa ziara hiyo, kutakuwa na mambo machache muhimu yatakayo jitokeza.

Lakini Taniguchi anaeleza kuwa Abe ni kiongozi pekee wa kigeni ambaye “Trump anaweza kutumia masaa kadhaa wa kadhaa bila ya kuandaa nukta za mazungumzo yake, na hicho kinafanya kuwepo mkakati wenye thamani kwa diplomasia ya Japan.

Alipoulizwa na VOA iwapo ziara hiyo itakuwa na tija ya kuwepo matokeo ya ushirikiano wa kibiashara na ulinzi, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani akieleza juu ya ratiba ya Trump na Abe ya Jumatatu juu ya kufanyika kwa mkutano na waandishi wa habari, “ watakuwa na matangazo yenye kuvutia sana juu ya kiwango cha mahusiano yao.”

XS
SM
MD
LG