Viongozi hao pia wametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yao.
Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa mkutano huo wa tatu unaohudhuriwa pia na Rais wa China Xi Jingping na Waziri Mkuu wa Japan Shinto Abe, Rais wa Rashia Vladimir Putin amesema kuendelea kwa nchi za dunia kulinda uchumi na masoko yao kunazusha changamoto kwa uchumi wa nchi za Asia.
Kiongozi huyo wa Rashia pia amesema kwamba Korea ya Kaskazini imechukua hatua za kuanza kuangamiza mpango wake wa nyuklia lakini Marekani haijajibu na inatoa masharti yasiyo malizika ya kuitaka kuangamiza kabisa silaha hizo.
Kwa upande wake Rais Xi wa China alitoa wito kwa viongozi wa Asia kuchukuwa juhudi za pamoja ili kuimarisha ustawi na uchumi wa kikanda.
Alisema nchi yake itaimarisha ushirikiano na Rashia katika kuleta maendeleo katika maeneo ya mashariki ya mbali ya Rashia na hivyo kusaidia maendeleo ya nchi za mashariki ya mbali.
Jopo hilo la ushirikaino wa kiuchumi wa Mashariki ya Mbali lilianzishwa na Rais Putin 2015, likiwa jukwa muhimu la kuwepo kwa mazungumzo ya ana kwa ana kati ya wanasiasa, wafanyabiashara na waatalamu kwa ajili ya maendeleo ya nchi za Mashariki ya Mbali, na ushirikiano wa kikanda.
Viongozi na wajumbe kutoka mataifa 60 wanahudhuria mkutano huo wa siku tatu wa Vladivostok.