Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:12

White House inatarajia mazungumzo ya Trump na Abe yatakuwa chanya


Rais wa Marekani, Donald Trump (L) na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe
Rais wa Marekani, Donald Trump (L) na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe

Ikulu ya Marekani ilisema inatarajia mazungumzo ya siku mbili kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe yatakuwa mazuri sana.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu ndani ya ndege maalumu ya rais ikielekea jimbo la Florida, msemaji wa White House, Sarah Huckabee Sanders alisema majadiliano kati ya viongozi hao wawili yatalenga zaidi juu ya maandalizi kwa mazungumzo na Korea kaskazini pamoja na majadiliano mengi juu ya biashara.

Rais Trump na Abe wanafahamiana. Waziri Mkuu wa Japan ni kiongozi wa kigeni ambaye Rais wa Marekani amekutana naye pamoja na kuzungumza naye mara nyingi wakati wa urais wake. Msemaji wa White House alisema Trump na Abe wana wasi wasi kuhusu Korea kaskazini ambayo ina program za makombora na silaha za nyuklia ikikaidi vikwazo vya kimataifa.

XS
SM
MD
LG