Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:03

Kim Jong Un ampokea kwa shangwe Moon Jae-in mjini Pyongyang


Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, pamoja na mkewe Kim Jung-sook, wakikaribishwa na kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un na mkewe Ri Sol Ju, Sept. 18, 2018.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, pamoja na mkewe Kim Jung-sook, wakikaribishwa na kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un na mkewe Ri Sol Ju, Sept. 18, 2018.

Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amepokelewa kwa heshima zote za kitaifa mjini Pyongyang siku ya Jumanne na mwenyeji wake Kim Jong Un aliyemkumbatia aliposhuka kutoka ndege yake na kukagua gwaride la kijeshi kwa pamoja.

Rais Moon Jae-in, wa korea Kusini, kushoto, akumbatiana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipowasili Pyongyang,
Rais Moon Jae-in, wa korea Kusini, kushoto, akumbatiana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipowasili Pyongyang,

Moon ananza ziara rasmi ya siku tatu Korea Kaaskazini ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Korea Kusini katika kipindi cha karibu muongo mmoja.

Huu ni mkutano wa tatu kati ya viongozi hao wawili tangu kukutana katika mkutano wa kihistoria mwezi April mwaka huu, kwenye kituo cha mpakani kati ya nchi zao cha Panmunjon.

Lengo kuu la ziara hii ni kujaribu kufufua tena majadiliano yaliyokwama ya kidiplomasia kati ya Marekani na Korea Kaskazini juu ya kuangamiza silaha zake za nuklia pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao.

Mchambuzi wa masuala ya Korea katika taasisi ya Asia kwa ajili ya taalum ya siasa, Chun Sung Hoon ameiambia Sauti ya Amerika kwamba suala la msingi ambalo jumia ya kimataifa inabidi kuzingatia kwenye mkutano huo wa kilele ni,

“ikiwa Kim Jong Un binafsi anadhamira na nia ya dhati kuachana kabisa na silaha za nuklia, na kurudi katika mkataba wa kutosambaza silaha za nuklia NPT na kua taifa lisilo miliki silaha za nuklia.”amesema Chun

Daniel Pinkston wa chuo kikuu cha Troy anasema kuna matarajio kadhaa wakati wa mkutano huu wa tatu, sio tu upande wa Korea ya Kusini bali pia Marekani na mataifa mengine katika kanda hiyo ya asia.

“Kuhusiana na kuchukuliwa hatua za kujenga hali ya kuaminiana upande wa masuala ya usalama, kuwepo na hatua za kupunguza silaha hasa upande wa nuklia na watu wanatarajia hatua za dhati zitakazo leta mabadiliko.”

Pinkston anasema Moon Jae-in akiwa rais wa tatu wa Korea Kusini kutembelea Pyongyang tangu kumalizika vita vya korea 1953 anakabiliwa na shinikizo kikubwa cha kumshawishi na kuhakikisha kiongozi mwenzake Kim Jon UN anachukua hatua za dhati kwa vitendo.

Kiongozi wa kwanza wa kusini kutembelea kaskazini alikua Kim dae Jung mwaka 2000 akifuatiwa na Roh Moo Hyun mwaka 2007.

Wakorea Kusini wakipepea bendera yao kumtakia rais wao mafanikio kwenye mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini, Sept. 18, 2018.
Wakorea Kusini wakipepea bendera yao kumtakia rais wao mafanikio kwenye mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini, Sept. 18, 2018.

Katika ziara hii nadra rais Moon anafuatana na ujumbe mkubwa wa watu 150 ambao ni wafanya biashara, maafisa wa michezo, sanaa na maafisa wa serikali.

Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA linaripoti kwamba mkutano huo wa kilele utatoa nafasi muhimu ya kuharakisha maendeleo katika ushirikaino kati ya Korea mbili ambao unaingia katika ukurasa mpya wa kihistoria.

XS
SM
MD
LG