Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazni linasema Kim anatarajia kushirikiana na Trump kwa nia njema ili kuweza kufikia malengo ya kila nchi hiyo.
Ahadi hiyo ya Kim inatokana na ziara ya makamu mwenyekiti wa chama tawala huko Korea Kaskazini Kim Yong Chol mjini Washington, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya mkutano huo.
Trump anataka ahadi thabiti kutoka Korea Kaskazini kuachana na silaha za nyuklia wakati Kim akiitaka jumuiya ya kimataifa kufuta vikwazo kwa nchi yake ili aweze kufanya kazi katika juhudi za kuinua uchumi wa nchi hiyo.