Wanajeshi hao wameanza shughuli ya kuondoa silaha katika vituo vya ulinzi mpakani, katika sehemu isiyo na shughuli za kijeshi.
Korea kaskazini ilishambulia upande wa kusini mwaka 1950 na kusababisha vita vya Korea, vilivyomalizika mwaka 1953 lakini vikaacha uhusiano mbaya wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Juhudi za kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo zimekuwa zikiendelea tangu mwanzoni mwa mwaka 2018.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na mwenzake wa Kaskazini Kim Jong Un mwenye silaha za nyuklia, walikubaliana mwezi Septemba, 2018 katika mkutano wao wa Pyongyang, kupunguza idadi ya vituo vya ulinzi mpakani. Nchi zote mbili zimeharibu vituo kumi hadi sasa.