Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:17

Marekani imewawekea vikwazo maafisa wa Korea Kaskazini


Steve Mnuchin, waziei wa fedha wa Marekani
Steve Mnuchin, waziei wa fedha wa Marekani

Marekani imewawekea vikwazo maafisa watatu waandamizi wa Korea Kaskazini kwa kile inachosema ni kuendelea kwa utawala katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na udhibiti.

Waziri wa fedha wa Marekani, Steve Mnuchin alisema kuwa maafisa hao watatu wanaendesha wizara ambao zinakiuka haki za binadamu, kukandamiza na kudhibiti raia. Marekani mara kwa mara imeushutumu utawala wa Korea Kaskazini kwa ukiukaji wake mkubwa na wa kikatili katika haki za binadamu na uhuru wa msingi alisema Mnuchin. Marekani pia imezuia mali zao na raia wa Marekani wamezuiliwa kufanya biashara nao.

Maafisa wa Marekani walisema Jumatatu kuwa vikwazo vipya pia ni ukumbusho kwa vitendo vya kikatili na kifo cha mwanafunzi wa chuo cha juu Mmarekani Otto Warmbier. Warmbier alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela mwaka 2016 kwa shutuma za wizi wakati wa ziara nchini Korea Kaskazini. Aliugua na kupoteza fahamu wakati akiwa chini ya ulinzi nchini humo na kufariki wiki moja baada ya kurejea Marekani.

XS
SM
MD
LG