Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:06

Korea Kaskazini : Ripoti mpya ya makombora itaathiri mazungumzo yajayo?


Eneo la Sino-ri, ambalo ni kituo cha kujeshi chenye makombora, Korea Kaskazini
Eneo la Sino-ri, ambalo ni kituo cha kujeshi chenye makombora, Korea Kaskazini

Ripoti iliyotolewa Jumatatu na kituo cha utafiti cha masuala ya mkakati na kimataifa – CSIS – kuhusu eneo ambalo halikutajwa mahali lilipo la makombora ya Korea Kaskazini la zamani inaeleza inawezekana lilikuwa limetambuliwa na waangalizi wa Korea Kaskazini bila ya kutarajia..

Lakini Nam Sung-wook, profesa katika Chuo Kikuu cha muungano, diplomasia na usalama cha Korea, amesema kituo hicho cha makombora cha Sino-ri kilikuwa siku za nyuma kinajulikana na idara za ujasusi za pande zote mbili Marekani na Korea Kusini.

Moja ya ripoti za zamani za Korea Kusini za kuanzia mwaka 1998 zinaeleza kuwa kituo cha Sino-ri ni cha makombora ya Nodong.

Ripoti hiyo ya CSIS imeeleza kwamba kituo kimoja kati ya 20 ambavyo Korea Kaskazini haijaviweka wazi vinatumika kama makao makuu ya sehemu za kuhifadhia makombora na kituo cha makombora ambayo yanafanya kazi.

Taarifa ya makombora aina ya Nodong ambayo yameandaliwa katika eneo hili zinalingana na kile kinacho aminika juu ya mikakati ya kijeshi ya silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini kwa kuweka tayari silaha za nyuklia zenye uwezo wa kushambulia katika hatua ya kwanza ya vita.

Kim Dong-yub, mkuu wa ofisi ya utafiti katika chuo cha tafiti za mashariki ya mbali (IFES) katika chuo kikuu cha Kyungnam, ameongeza kuwa, “Ijapokuwa Korea Kaskazini haijatangaza rasmi eneo hilo la makombora, haimanishi kuwa hilo ni eneo jipya. Hakuna nchi inayotangaza vituo vyake yote ya kijeshi

Nam ameeleza kuwa Marekani inaangaza vipengele vidogo kwa undani zaidi juu ya kutokomeza kwa silaha za nyuklia, kama vile kuangamiza makombora ya balistiki yanayo weza kufika mabara mengine (ICBM) ili kupunguza vitisho dhidi ya Marekani. Kwa upande wake [Rais] Trump, anaweza kutumia hoja hii kujigamba juu ya mafanikio yake wakati wa mkutano wa pili,” amesema Nam.

XS
SM
MD
LG