Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:55

Mkutano wa Hanoi :Trump akanusha uvumi kuwa hatatekeleza ahadi yake


Rais Trump akipeana mkono na Kiongozi Kim kabla ya mkutano wao huko Hanoi, Februari 27, 2019.
Rais Trump akipeana mkono na Kiongozi Kim kabla ya mkutano wao huko Hanoi, Februari 27, 2019.

Akiwa amesimama mbele ya bendera ya Marekani na Korea Kaskazini akipeana mikono na Kim Jong Un, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wao wa pili, Rais wa Marekani Donald Trump amekanusha uvumi kwamba amerudi nyuma katika kutekeleza ahadi yake ya kutokomeza silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea.

Alipoulizwa na waandishi iwapo watatoa tamko la kutangaza rasmi kumalizika kwa Vita vya Korea, ambavyo vilisitishwa kwa kufikia makubaliano ya amani mwaka 1953, Trump alijibu kuwa “Tutaangalia hilo.”

Kiongozi wa Korea Kaskazini na Trump – kabla ya karamu ya chakula cha usiku – mara moja waliingia katika chumba pembeni katika Hoteli ya Hanoi Metropole ambako wanafanya mkutano mfupi pamoja na wakalimani wao.

Kikundi kidogo cha waandishi, kilichoingia katika chumba cha mazungumzo, walimsikia Kim akimpongeza Trump kwa “maamuzi yake ya kijasiri” kwa kuwepo mazungumzo yao, yaliyokuwa yameanza mwaka jana nchini Singapore.

“Tulipiga hatua ya kutosha na nafikiri maendeleo makubwa kuliko yote ni maelewano yetu ambayo kwa kweli ni mazuri,” Trump amesema kumwambia Kim.

Pia amesifia mapokezi yao huko Vietnam “kwa kweli wametutandikia zulia jekundu" katika makaribisho hayo ya mkutano wao huu unaofuatia ule wa kwanza, akiongeza kuwa anamatumaini mkutano huu unalingana na ule wa kwanza au mkubwa zaidi.

Imetayrishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG