Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:50

Rais Trump na Kim Jong Un wamewasili Singapore


Kim Jong Un wa Korea kaskazini (L) na Rais wa marekani, Donald Trump
Kim Jong Un wa Korea kaskazini (L) na Rais wa marekani, Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini wamewasili mjini Singapore katika kile ambacho kinachukuliwa kuwa mkutano wa kwanza kuwahi kutokea kati ya viongozi hao walio madarakani wa mataifa haya mawili.

Mkutano huo wa kihistoria utafanyika Jumanne Juni 12 chini ya ulinzi mkali na matumaini makubwa kutoka pande mbili na dunia nzima inasubiri kwa hamu kuona kitakachotokea.

Hii ni mara ya kwanza Kim Jong Un kusafiri mbali kutoka nchini mwake tangu kuchukua madaraka mwaka 2011.

Trump ameueleza mkutano wa June 12 kama jaribio la mara moja la kupatikana amani, lakini haifahamiki ni masuala gani hasa yaliyoko kwenye ajenda ya mazungumzo.

Dunia ikisubiri mkutano wa Trump na Kim Jong Un kupitia TV
Dunia ikisubiri mkutano wa Trump na Kim Jong Un kupitia TV

Kwa hivyo macho yote ya dunia yapo Singapore kwa kile ambacho huwenda kikadhihirisha kuwa mkutano muhimu wa nyuklia wa dunia kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa vita baridi. Matarajio ya Washington yapo juu huku zikihesabiwa saa kadhaa zijazo kwa wawili hao kuanza majadiliano.

Mkutano wa ana kwa ana kwa viongozi hao wasiotabirika ambapo kila mmoja alitishia kuharibu nchi ya mwenzie kabla hawajakubaliana kwenda kwenye mkutano ambao umeshangaza dunia. Rais Trump alisema atafahamu katika dakika ya kwanza ikiwa makubaliano yataweza kufikiwa na Kim Jong Un.

Trump alisema “Nitakuwa kwenye kazi ya kutafuta amani. Huwenda isifanikiwe, kuna nafasi kubwa huwenda jambo hili lisifanikiwe. Huwenda pia kuna nafasi nzuri zaidi kwamba jambo hili litachukua muda litakua ni utaratibu”.

Wakati huo huo, seneta M-Republican Lindsey Graham alisema mkutano wa Trump na Kim utafungua njia ya kufikiwa makubaliano ambayo Korea kaskazini inaachana na program zake za nyuklia na makombora ya masafa ya mbali, ili nayo iweza kuhakikishiwa uasalama wake. Lakini Graham anashinikiza kuwepo na mpango mbadala wa dharura kama mazungumzo yanashindikana, kupatikana idhini ya bunge la Marekani ili kutumia nguvu za jeshi dhidi ya korea kaskazini.

“Kama diplomasia itashindwa kama njia ya mwisho, wademocrat na warepublican wanahitajika kupendekeza suluhisho la kijeshi la sivyo hatutapata kamwe mkataba mzuri”.

XS
SM
MD
LG