Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 12:57

Wakulima Uhispania wameandamana kufuatia mgogoro katika sekta ya kilimo


Wakulima wa Uhispania wanaandamana kufuatia mzozo uliopo kwenye sekta ya kilimo. Spain, Feb. 7, 2024.
Wakulima wa Uhispania wanaandamana kufuatia mzozo uliopo kwenye sekta ya kilimo. Spain, Feb. 7, 2024.

Ni baada ya Umoja wa Ulaya kupendekeza mabadiliko ya sheria kupunguza kwa kiasi kikubwa kanuni za mazingira za CAP

Mamia ya wakulima waliandamana katika mji mkuu wa Uhispania kwa miguu na kwa kutumia trekta siku ya Jumapili katika maandamano ya hivi karibuni kufuatia mgogoro unaoikabili sekta ya kilimo.

Wakulima waliandamana kutoka Wizara ya Mazingira kwenda Wizara ya Kilimo baada ya Umoja wa Ulaya kupendekeza mabadiliko ya sheria ili kupunguza kwa kiasi kikubwa kanuni za mazingira za Common Agricultural Policy (CAP) hapo Ijumaa.

Wakiandamana kutokana na muungano wao wa wafanyakazi, wakulima walibeba mabango yanayosomeka “Sisi sio wahalifu” huku wakipiga ngoma na filimbi. Mkulima mmoja alipamba trekta lake kwa michoro ya kejeli. “Kama wanataka kukata shingo zetu,” alisema Marcos Baldominos akiuelezea mchoro wake.

Forum

XS
SM
MD
LG