Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:00

Wanaharakati wa mazingira wajitokeza kwenye mkutano wa IAEA


Wanaharakati wa mazingira ikiwemo GreenPeace wakiandamana wakati mkutano wa Nishati ya Nyuklia wa IAEA ukiendelea huko Brussels.
Wanaharakati wa mazingira ikiwemo GreenPeace wakiandamana wakati mkutano wa Nishati ya Nyuklia wa IAEA ukiendelea huko Brussels.

Wanaharkati wa mazingira, ikiwemo GreenPeace, walifanya maandamano katika mkutano wa Nishati ya Nyuklia wa IAEA ulifoanyika leo mjini Brussels, na kutaka lengo liwe katika vyanzo vya nishati mbadala.

Viongozi kutoka nchi za Ulaya zinazounga mkono Nyuklia na watalaamu wa nishati wanapanga kutoa wito katika mkutano huo kufufuliwa kwa nishati ya nyuklia, wakitaka kujengwa tena kwa sekta hiyo huko Ulaya baada ya kushuka kwa miaka kadhaa.

Nyuklia iliacha kuwa ni kipaumbele huko Ulaya kwasababu ya wasiwasi wa usalama kufuatia ajali ya nyuklia huko Fukushima nchini Japan mwaka 2011, ambayo iliichochea Ujerumani haraka kufunga viwanda vyake sita vya nyuklia na kuondoa vinu vyake vilivyobaki. Viwanda vitatu vya mwisho vilifungwa April mwaka 2023.

Lakini haja ya kubuni njia mbadala kwa gesi za Russia kunafuatia uvamizi wa Moscow nchini Ukraine mwaka 2022, na nia ya dhati ya Umoja wa Ulaya kupunguza uchafuzi utokanao na gesi chafu kwa asilimia 55 ifikapo mwaka 2030 kumefufua maslahi mapya kwa nishati ya nyuklia.

Hata hivyo nchi za EU bado zimegawanyika juu ya iwapo wahamasishe nishati ya nyuklia, huku kukiwa na kambi mbili – moja ikiongozwa na Ufaransa ambayo inaamini upanuzi wa nyuklia ni muhimu na nyingine ikiwa ni zile nchi ambazo zinapinga nyuklia Austria na Ujerumani, ambao wanataka kulenga kubaki katika vyanzo vya nishati mbadala kama vile upepo na nishati ya jua.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG