Rais Joe Biden amesifia makubaliano yaliyotiwa saini katika mkutano wa COP 28 kama hatua muhimu kuelekea kufikia malengo ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Biden alipongeza makubaliano hayo ambayo kwa mara ya kwanza yamejikita katika kuondoka kwenye matumizi ya mafuta ghafi akisema yanahatarisha sayari na watu wetu, kukubali kuongeza mara tatu nishati mbadala duniani kote, ifikapo 2030, na zaidi ya hapo.
Rais alisema, hata hivyo bado kuna kazi kubwa siku za mbele ya kuweka lengo la kufikia digrii 1.5 C kuwezekana.
Wajumbe kutoka nchi karibu 200 walikubaliana mapema jumatano katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa huko Dubai kuondokana na matumizi ya mafuta ghafi.
Makubaliano hayo yamekuja baada ya wiki mbili za mazungumzo yaliyolenga chanzo kikuu kinachosababisha uzalishaji wa gesi chafu duniani.
Forum