Shauri la iwapo dunia inapaswa kwa mara ya kwanza kabisa kukubaliana kumaliza enzi za matumizi ya nishati ya mafuta limekuwa kiini cha mkutano huo wa kimataifa ambapo takribani nchi 200 zinajaribu kufikia muafaka wa mabadiliko ya hali ya hewa.
Muungano wa zaidi ya nchi 80 zikiwemo Marekani, Umoja wa Ulaya, na mataifa ya visiwa vidogo ulishinikiza makubaliano ambayo yanajumuisha msimamo wa kuondoa mafuta, gesi, na makaa ya mawe kama nishati za msingi lakini walikabiliwa na upinzani mkali unaoongozwa na kundi la wazalishaji mafuta OPEC na washirika wake.
Forum