Mashauriano ya karibuni kuelekea mkataba wa kimataifa wa kupambana na uchafuzi wa plastiki yalianza jijini Nairobi leo Jumatatu, huku mivutano ikitarajiwa wakati mataifa yakilumbana juu ya nani anapaswa kujumuishwa katika mkataba huo.
Nchi zipatazo 175 zilikubaliana mwaka jana kukamilisha ifikapo mwaka 2024 mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia masuala ya plastiki katika bahari, na zile zinazoelea kwenye ukanda huo na kujipenyeza kwenye miili ya wanyama na binadamu.
Ingawa kuna makubaliano mapana kwamba mkataba unahitajika, kuna maoni mseto juu ya kile kinachopaswa kuwa ndani yake. Wakati mazungumzo hayo yakifunguliwa rasmi, Gustavo Meza-Cuadra Velasquez mwenyekiti wa kamati ya majadiliano ya serikali katika nchi hizo alionya kuwa uchafuzi wa plastiki unaleta tishio la moja kwa moja kwa mazingira yetu, afya ya binadamu, na usawa wa sayari yetu.
Forum