Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 16:50

UN yatoa wito wa kushughulikia kwa haraka mzozo wa Sudan


Picha hii ya Amnesty International yaonyesha mbunge wa California Sara Jacobs akizungumza katika kampeni ya mshikamano na Sudan, Washington Aprili 15, 2024.
Picha hii ya Amnesty International yaonyesha mbunge wa California Sara Jacobs akizungumza katika kampeni ya mshikamano na Sudan, Washington Aprili 15, 2024.

Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kushughulikia mzozo wa Sudan unaozidi kuwa mbaya, akisisitiza mateso kwa mamilioni ya watu waliokoseshwa makazi kutokana na mzozo huo.

Tom Fletcher alizungumza na wakimbizi wakati wa ziara ya siku tisa nchini Sudan na Chad, akiapa kupaza sauti zaidi kwa kuwatetea na kuutaka ulimwengu kutoa msaada mkubwa zaidi.

“Sisi hatuonekani,” alisema, akiwasilisha ujumbe kutoka kwa walioathirika.

Sudan imetumbukia katika vita tangu Aprili 2023, vinavyolihusisha jeshi la serikali linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces( RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo.

Machafuko yameua maelfu ya watu na kuwakosesha makazi zaidi ya watu milioni 11, na kusababisha kile Umoja wa Mataifa umekielezea kama mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu katika historia ya hivi karibuni.

Forum

XS
SM
MD
LG