Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:42

Kais Saied atarajiwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais nchini Tunisia


Rais wa Tunisia Kais Saied akipiga kura katika uchaguzi wa rais mjini Tunis, Oktoba 6, 2024.
Rais wa Tunisia Kais Saied akipiga kura katika uchaguzi wa rais mjini Tunis, Oktoba 6, 2024.

Rais wa Tunisia aliye madarakani Kais Saied anatarajiwa kushinda uchaguzi wa rais nchini humo kwa asilimia 89.2 licha ya idadi ndogo ya wapiga kura, kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa Jumapili kwenye televisheni ya taifa baada ya upigaji kura kumalizika.

Saied mwenye umri wa miaka 66, anatarajiwa kupata ushindi wa kishindo, na kuwashinda wapinzani wake, mpinzani aneyefungwa jela Ayachi Zammel, ambaye anatarajiwa kupata asilimia 6.9 ya kura, na Zouhair Maghzaoui, akitarajiwa kupata asilimia 3.9, lilisema kundi huru linalofuatilia uchaguzi la Sigma Conseil.

Miaka mitatu baada ya Saied kujinyakulia mamlaka makubwa, makundi ya kutetea haki za binadamu yanahofia kuchaguliwa kwake kwa muhula mwingine kutaimarisha zaidi utawala wake nchini humo, demokrasia iliyoimarika kutokana na maandamano ya mapinduzi ya nchi za Kiarabu, maarufu Arab Spring.

Baada ya kuondolewa madarakani dikteta wa muda mrefu Zine El Abidine Ali mwaka 2011, Tunisia ilijivunia kuwa kitovu cha maandamano ya kikanda dhidi ya utawala wa kimabavu.

Lakini mwelekeo wa taifa hilo la Afrika Kaskazini ulibadilika vibaya muda mfupi baada ya kuchaguliwa kwa Saied mwaka 2019.

Tume ya uchaguzi ya Tunisia, ISIE, ilesema watu milioni 9.7 walitarajiwa kupiga kura, katika nchi yenye watu milioni 12.

Asilimia 27.7 tu ya wapiga kura ndio walijitokeza kupiga kura, tume ya uchaguzi ilisema. Zaidi ya asilimia 58 walikuwa wanaume, na asilimia 65 walikuwa na umri wa kati ya miaka 36 na 60.

Forum

XS
SM
MD
LG