Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 23:31

Chama cha upinzani nchini Namibia kinaomba zoezi la kuhesabu kura lisitishwe


Afisa wa tume ya uchaguzi ya Namibia akihesabu kura kwenye kituo cha kupigia kura kwenye chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia mjini Windhoek, Novemba 28, 2024. Picha ya AFP
Afisa wa tume ya uchaguzi ya Namibia akihesabu kura kwenye kituo cha kupigia kura kwenye chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia mjini Windhoek, Novemba 28, 2024. Picha ya AFP

Chama cha upinzani nchini Namibia Alhamisi kimeomba zoezi la kuhesabu kura lisitishwe baada ya uchaguzi wa taifa kukabiliwa na changamoto za kiufundi na upigaji kura kuendelea baada ya muda wa kufungwa kwa vituo vya kupigia kura.

Uchaguzi wa rais na bunge ni mtihani mkubwa kwa chama tawala cha SWAPO ambacho kimetawala katika taifa hilo lenye utajiri wa madini tangu lijipatie uhuru miaka 34 iliyopita na kinakabiliwa na uchaguzi wenye upinzani mkali.

Baadhi ya wapiga kura walikuwa kwenye foleni usiku baada ya mamlaka kuruhusu vituo vya kupigia kura kufunguliwa baada ya muda uliopangwa wa kuvifunga saa tatu usiku siku ya Jumatano kutokana na kuwa watu wengi sana walikuwa bado wakisubiri kupiga kura.

Baadhi ya vituo vya kupigia kura vilianza hata hivyo kuhesabu kura.

“Kuna vituo vya kupigia kura ambavyo vimeanza kutangaza matokeo, kuna vituo vya kupigia kura ambavyo vinatwambia viliamrishwa kusitisha zoezi la kuhesabu kura,” alisema Christine Aoachamus kutoka chama kikuu cha upinzani, Independent Patriots for Change(IPC).

Forum

XS
SM
MD
LG