Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 05:43

Amnesty inaomba kuundwe tume ya kuchunguza mauaji yanayohusiana na maandamano ya Kenya


Tamasha la kuwakumbuka watu waliouawa katika maandamano ya kupinga nyongeza ya ushuru nchini Kenya, Julai 7, 2024. Picha ya Reuters
Tamasha la kuwakumbuka watu waliouawa katika maandamano ya kupinga nyongeza ya ushuru nchini Kenya, Julai 7, 2024. Picha ya Reuters

Miezi mitatu baada ya maandamano makubwa dhidi ya serikali nchini Kenya, shirika la haki za binadamu Amnesty International linatarajiwa kuwasilisha ombi leo Jumatano ili kuundwe tume itakayochunguza vifo vya watu kadhaa kutokana na “polisi kutumia nguvu kupita kiasi kinyume cha sheria.”

Haya yanajiri baada ya akina mama wazazi wa waandamanaji kukusanyika nje ya wizara ya sheria Jumanne kuwasilisha orodha ya waliouawa katika msururu wa maandamano yaliyofanyika kati ya mwezi Juni na Agosti.

“Tunachotaka kwa serikali yetu ni haki,” alisema Caroline Mutisya, ambaye alimpoteza mwanawe Erikson Kyalo.

Alisema “Tunataka maafisa wote wa polisi waliowauwa watu wakamatwe.”

Makundi ya haki za binadamu yanasema zaidi ya watu 60 waliuawa wakati wa wiki kadhaa za maandamano, yaliyochochewa awali na mswada wa fedha uliopendekeza nyongeza ya ushuru, huku wengine wakitoweka wiki kadhaa baada ya maandamano.

Maandamano ya amani yaliyoongozwa na vijana dhidi ya pendekezo la nyongeza ya ushuru yalichochea upinzani mkubwa dhidi ya rais William Ruto na kile ambacho wengi wanaona kama matumizi mabaya ya fedha za umma na ufisadi.

Forum

XS
SM
MD
LG