Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 19, 2025 Local time: 06:16

Seneta wa zamani wa Marekani ahukumiwa kifungo cha miaka 11


Seneta wa zamani wa Marekani Bob Menendez akifika kwenye Mahakama ya serikali kuu ya Manhattan, Mei 13, 2024. Picha ya AFP
Seneta wa zamani wa Marekani Bob Menendez akifika kwenye Mahakama ya serikali kuu ya Manhattan, Mei 13, 2024. Picha ya AFP

Jaji Jumatano amemhukumu seneta wa zamani wa Marekani mwenye ushawishi mkubwa kifungo cha miaka 11 jela, baada ya kukutwa na hatia ya rushwa kufuatia kugunduliwa kwa dhahabu nyingi na maelfu ya dola pesa taslimu nyumbani kwake.

Robert Menendez, mwenye umri wa miaka 71, Mdemocrat kutoka jimbo la New Jersey, alikutwa na hatia ya ulaghai, kutatiza kazi ya vyombo vya sheria na kupokea hongo ili kuwapendelea wafanyabiashara wenye uhusiano na Misri na Qatar.

“Mahali fulani njiani, umepotea njia,” Jaji Sidney Stein alisema akitangaza hukumu ya kifungo cha miaka 11.

“Badala ya kufanya kazi kwa manufaa ya umma, ilibadilika kufanya kazi kwa ajili ya manufaa yako.”

Menendez, ambaye alihudumu kama mwenyekiti wa Kamati ya masuala ya kigeni katika Baraza la Seneti, aliapa kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa Julai 2024, na Jumatano alimuomba msamaha jaji huyo kabla ya hukumu dhidi yake.

Forum

XS
SM
MD
LG