Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 22:39

Waasi wa M23 waelekea Kivu Kusini baada ya kuuteka mji wa Goma


Waasi wa M23 wakifanya doria katika mitaa ya mji wa Goma, Januari 29, 2025. Picha ya AP
Waasi wa M23 wakifanya doria katika mitaa ya mji wa Goma, Januari 29, 2025. Picha ya AP

Kundi la waasi wa M23 limesonga mbele kwenye uwanja mwingine wa mapambano huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa kuteka wilaya mbili katika jimbo la Kivu Kusini, vyanzo vya eneo hilo vimeiambia AFP Jumatano.

Kundi hilo limesonga mbali zaidi baada ya kuchukua udhibiti wa mji muhimu wa Goma huko Kivu Kaskazini kufuatia mapigano makali na wanajeshi wa Congo.

Jumatano asubuhi, waasi wa M23 hawakupata usumbufu wowote kwa kuteka wilaya za Kiniezire na Mukwidja katika jimbo jirani la Kivu Kusini, chanzo cha maeneo hayo na wakazi wamesema.

“Hapakuwa mapigano” wakati wakisonga mbele, amesema kiongozi wa mashirika ya kiraia ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama.

Wakazi kadhaa wa vijiji hivyo viwili waliowasiliana na AFP wamethibitisha kutekwa kwa eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG