Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 20:53

Burkina Faso, Mali na Niger zaondoka rasmi kwenye ECOWAS


Viongozi wa kijeshi wa Niger, Mali na Burkina Faso wakikutana katika mkutano wa kwanza wa shirikisho lao mjini Niamey, Julai 6, 2024. Picha ya Reuters
Viongozi wa kijeshi wa Niger, Mali na Burkina Faso wakikutana katika mkutano wa kwanza wa shirikisho lao mjini Niamey, Julai 6, 2024. Picha ya Reuters

Maelfu ya watu katika nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zinazoongozwa na serikali za kijeshi Jumanne waliandamana kuunga mkono uamuzi wa nchi hizo wa kujiondoa kwenye Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Hatua hiyo inaanza kutekelezwa leo Jumatano.

Kuondoka kwa nchi hizo tatu ambazo zilianzisha jumuia hiyo kulisababisha mpasuko katika kanda hiyo na kuicha ECOWAS na mstakabali usio na uhakika.

Nchi hizo tatu ziliunda shirikisho tofauti linaloitwa Alliance of Sahel States (AES).

Ziliifamisha rasmi ECOWAS kuhusu mpango wao wa “kuondoka mara moja” mwezi Januari mwaka 2024, zikidai kwamba jumuia hiyo inaitegemea hasa Ufaransa kupita kiasi.

Paris iligeuka adui wa pamoja wa serikali hizo tatu za kijeshi, ambazo zinapendelea kushirikiana na nchi kama Russia, Uturuki na Iran.

Hata hivyo, ECOWAS iliomba taarifa ya maandishi ya mwaka mmoja ili hatua ya kuondoka kwa nchi hizo itekelezwe, na tarehe ya mwisho imefika leo Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG