Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:07

UN: Watu milioni moja wamekimbilia Sudan Kusini

 Kambi ya Wakimbizi waliokimbia vita Sudan ya Ourang , Adre Decemba 7, 2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP.
Kambi ya Wakimbizi waliokimbia vita Sudan ya Ourang , Adre Decemba 7, 2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP.

Maelfu ya watu wameuwawa na wengine zaidi ya milioni 12 wamekoseshwa makazi kutokana na mzozo uliozuka baina ya jeshi la Sudan na kundi la waasi tangu April mwaka 2023.

Zaidi ya watu laki saba wamekimbia kupitia kivuko cha mpakani cha Joda katika kipindi cha miezi 21 iliyopita wakati maelfu ya watu wengine wamevuka na kuingia Sudan Kusini na kwingineko.

Wimbi hili la wakimbizi limefikisha jumla ya idadi ya watu waliokimbia kufikia zaidi ya milioni moja kwa mujibu wa taarifa za Umoja wa Mataifa.

Watu wakivuka mpaka kutoka Sudan kwenda Sudan Kusini kwa mkokoteni unaovutwa na punda wakipokelewa na maafisa wanaofuatilia wakimbizi katika mpaka wa Joda, Sudan Kusini. (AP Photo/Sam Mednick)
Watu wakivuka mpaka kutoka Sudan kwenda Sudan Kusini kwa mkokoteni unaovutwa na punda wakipokelewa na maafisa wanaofuatilia wakimbizi katika mpaka wa Joda, Sudan Kusini. (AP Photo/Sam Mednick)

Mamilioni ya watu wengi wanaovuka mpaka ni raia wa Sudan Kusini ambao awali walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo changa, shirika la kuhudumia wakimbizi la UNHCR limesema katika taarifa yake.

Taarifa ya Pamoja ya UN imetoa wito wa kuongezwa misaada zaidi kwa watu wote waliokoseshwa makazi na watu wanaowahifadhi , wakionya kwamba rasilimali za sudan kusini kama vile huduma za afya , maji na makazi zimetumika sana .

Forum

XS
SM
MD
LG