Shirika la misaada ya matibabu- MSF lilisema Ijumaa limelazimika kusimamisha shughuli zake katika mojawapo ya hospitali chache zilizosalia kusini mwa Khartoum kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara, na kukatika kwa njia nyingine ya kuokoa maisha kwa wale waliobaki katika mji mkuu wa Sudan.
Vita vimekuwa vikiendelea nchini Sudan tangu Aprili mwaka 2023, vilichochewa na mapambano ya madaraka kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya dharura (RSF) kabla ya mpango wa mpito kuelekea utawala wa kiraia, na kusababisha mzozo mkubwa sana wa ukosefu wa makazi na njaa.
Hospitali, ambayo iko katika eneo linalodhibitiwa na RSF, ilisaidia kuwatibu waathirika wa mashambulizi ya anga ya mara kwa mara ya Jeshi la Sudan, pamoja na mamia ya wanawake na watoto wenye utapiamlo katika eneo ambalo vitongoji viwili vimetumbukizwa katika hatari ya njaa.
Forum