Maandamano yalizuka katika mji mkuu wa Juba wiki iliyopita kutokana na ripoti kwamba mapigano katika nchi jirani ya Sudan yaliua raia 29 wa Sudan Kusini, lakini yaligeuka vurugu huku watu wakipora maduka ya biashara yanayomilikiwa na raia wa Sudan.
Hasira ilienea katika taifa hilo maskini, huku maafisa wa usalama wakifyatua risasi kutawanya umati wa watu na baadaye kuwashikilia mamia ya waporaji.
Katika barua iliyowasilishwa kwa kampuni zinazotoa huduma ya intaneti nchini humo, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya kitaifa ya Mawasiliano (NCA) aliziamuru “kuzuia akaunti zote za mitandao ya kijamii kuanzia usiku wa manane Januari 22, 2025, kwa siku 90.”
Hatua hiyo ilithibitishwa baadaye na kampuni tatu za mawasiliano zinazofanya kazi nchini Sudan Kusini, ingawa hadi Jumatano jioni waandishi wa habari wa AFP bado walikuwa wanaweza kutumia Facebook nchini humo.
Mkurugenzi mkuu wa NCA Napoleon Adok alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya “machafuko ya hivi karibuni nchini Sudan, ambayo yamewaweka raia wa Sudan Kusini kwenye hali ya ukatili wa hali ya juu kupitia mitandao ya kijamii.”
Aliongeza kuwa raia nchini Sudan “walikabiliwa na mashambulizi mabaya yaliyosababisha vifo vya wanawake na Watoto, na baadaye kurikodiwa kwenye video na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii bila kujali.”
Forum