Waziri mkuu Benjamin Netanyahu anakibiliwa na shinikizo kubwa ili mateka wanaosalia waweze kuachiliwa baada ya Waisrael watatu walioachiliwa siku ya Jumamosi kurejea nyumbani wakiwa katika hali dhaifu baada ya kushikiliwa na Hamas kwa kipindi cha miezi 16.
Katika ishara nyingine inayoonyesha kuwa sitisho la mapigano lipo katika hali tete, jeshi la Israel lilisema Jumatatu jioni kwamba limefuta likizo kwa wanajeshi waliopelekwa Gaza.
Hamas ilisema mpango wake wa kuchelewesha awamu nyingine ya kuwaachilia mateka “hadi kutakapotolewa taarifa nyingine” inategemea ikiwa Israel “itatekeleza wajibu wake.”
Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kwamba ikiwa mateka wote wanaoshikiliwa huko Gaza hawataachiliwa ifikapo Jumamosi alasiri, atapendekeza makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas yavunjwe “na kuacha hatua zote kali zichukuliwe.”
Forum