Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 19:42

Mapigano yazuka karibu na mji wa Bukavu, Kivu Kusini


Waasi wa M23 wakifanya doria katika mitaa ya Goma, Januari 29, 2025. Picha ya AP
Waasi wa M23 wakifanya doria katika mitaa ya Goma, Januari 29, 2025. Picha ya AP

Mapigano yalizuka Jumanne mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, siku tatu baada ya wito wa viongozi wa Afrika wa kusitisha mapigano na utulivu kwa muda mfupi katika mzozo huo.

Waasi wa M23 ambao inasemekana wanaungwa mkono na Rwanda walishambulia vituo vya jeshi la Congo katika jimbo la Kivu Kusini nyakati za alfajiri, vyanzo vya usalama na vya eneo hilo viliiambia AFP.

Mapigano hayo mapya yanatokea baada ya viongozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki kuomba wakuu wa majeshi yao kupendekeza mpango ili kutekeleza sitisho la mapigano “bila masharti” ifikapo Alhamisi, katika mzozo ambao umeua maelfu ya watu na kuondoa idadi kubwa ya watu kwenye makazi yao.

Kundi hilo lenye silaha lilianza kusonga mbele kuelekea Kivu Kusini baada ya kuchukua udhibiti wa Goma, mji mkuu wa jimbo jirani la Kivu Kaskazini ambalo linapakana na Rwanda, mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mapigano yalifanyika Jumanne karibu na kijiji cha Ihusi, kwenye umbali wa kilomita 70 kutoka mji mkuu wa Bukavu na umbali wa kilomita 40 kutoka Uwanja wa ndege wa jimbo, kulingana na vyanzo vya usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG