Tume ya Liberia ya kupambana na ufisadi (LACC) iligundua maafisa 457, akiwemo waziri anayesimamia bajeti pamoja na mabalozi, kuwa hawakutangaza mali zao kabla ya tarehe ya mwisho ya mwezi Novemba, kama inavyoagizwa na kanuni za maadili za nchi kwa maafisa wa serikali.
Maafisa hao “wamesimamishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja bila malipo hadi watakapowasilisha nyaraka zinazohitajika”, ofisi ya rais ilisema.
Sheria ya Liberia inawataka watumishi wa umma kutangaza mali zao wanapoingia au kuondoka kwenye nyadhifa zao.
Forum